1. BWANA, moyo wangu hauna kiburi,Wala macho yangu hayainuki.Wala sijishughulishi na mambo makuu,Wala na mambo yashindayo nguvu zangu.
2. Hakika nimeituliza nafsi yangu,Na kuinyamazisha.Kama mtoto aliyeachishwaKifuani mwa mama yake;Kama mtoto aliyeachishwa,Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu.