1. Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi,Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.
2. Katika miti iliyo katikati yakeTulivitundika vinubi vyetu.
3. Maana huko waliotuchukua matekaWalitaka tuwaimbie;Na waliotuonea walitaka furaha;Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.
4. Tuuimbeje wimbo wa BWANAKatika nchi ya ugeni?
5. Ee Yerusalemu, nikikusahau wewe,Mkono wangu wa kuume na usahau.
6. Ulimi wangu na ugandamaneNa kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka.Nisipoikuza YerusalemuZaidi ya furaha yangu iliyo kuu.
7. Ee BWANA, uwakumbuke wana wa Edomu,Siku ya Yerusalemu.Waliosema, Bomoeni!Bomoeni hata misingini!
8. Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia,Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi.