Zab. 95 Swahili Union Version (SUV)

Mwito wa Kuabudu na Kutii

1. Njoni, tumwimbie BWANA,Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.

2. Tuje mbele zake kwa shukrani,Tumfanyie shangwe kwa zaburi.

3. Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu,Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.

4. Mkononi mwake zimo bonde za dunia,Hata vilele vya milima ni vyake.

5. Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya,Na mikono yake iliumba nchi kavu.

6. Njoni, tuabudu, tusujudu,Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.

7. Kwa maana ndiye Mungu wetu,Na sisi tu watu wa malisho yake,Na kondoo za mkono wake.Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!

8. Msifanye migumu mioyo yenu;Kama vile huko MeribaKama siku ya Masa jangwani.

9. Hapo waliponijaribu baba zenu,Wakanipima, wakayaona matendo yangu.

10. Miaka arobaini nalihuzunika na kizazi kile,Nikasema, Hao ni watu waliopotoka mioyo,Hawakuzijua njia zangu.