Zab. 120 Swahili Union Version (SUV)

Sala ya Ukombozi

1. Katika shida yangu nalimlilia BWANANaye akaniitikia.

2. Ee BWANA, uiponye nafsi yanguNa midomo ya uongo na ulimi wa hila.

3. Akupe nini, akuzidishie nini,Ewe ulimi wenye hila?

4. Mishale ya mtu hodari iliyochongoka,Pamoja na makaa ya mretemu.

5. Ole wangu mimi!Kwa kuwa nimekaa katika Mesheki;Na kufanya maskani yanguKatikati ya hema za Kedari.

6. Nafsi yangu imekaa siku nyingi,Pamoja naye aichukiaye amani.