Zab. 124 Swahili Union Version (SUV)

Shukrani kwa Ukombozi wa Israeli

1. Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,Israeli na aseme sasa,

2. Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi,Wanadamu walipotushambulia.

3. Papo hapo wangalitumeza hai,Hasira yao ilipowaka juu yetu

4. Papo hapo maji yangalitugharikisha,Mto ungalipita juu ya roho zetu;

5. Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetuMaji yafurikayo.

6. Na ahimidiwe BWANA;Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao.

7. Nafsi yetu imeokoka kama ndegeKatika mtego wa wawindaji,Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.