Zab. 113 Swahili Union Version (SUV)

Mungu Msaidizi wa Mhitaji

1. Haleluya.Enyi watumishi wa BWANA, sifuni,Lisifuni jina la BWANA.

2. Jina la BWANA lihimidiweTangu leo na hata milele.

3. Toka maawio ya jua hata machweo yakeJina la BWANA husifiwa.

4. BWANA ni mkuu juu ya mataifa yote,Na utukufu wake ni juu ya mbingu.

5. Ni nani aliye mfano wa BWANA,Mungu wetu aketiye juu;

6. Anyenyekeaye kutazama,Mbinguni na duniani?

7. Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,Na kumpandisha maskini kutoka jaani.

8. Amketishe pamoja na wakuu,Pamoja na wakuu wa watu wake.