Zab. 125 Swahili Union Version (SUV)

Usalama wa Watu wa Mungu

1. Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni,Ambao hautatikisika, wakaa milele.

2. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu,Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake,Tangu sasa na hata milele.

3. Kwa maana fimbo ya udhalimuHaitakaa juu ya fungu la wenye haki;Wenye haki wasije wakainyoshaMikono yao kwenye upotovu.

4. Ee BWANA, uwatendee mema walio wema,Nao walio wanyofu wa moyo.