Zab. 134 Swahili Union Version (SUV)

Sifa ya Usiku

1. Tazama, enyi watumishi wa BWANA,Mhimidini BWANA, nyote pia.Ninyi mnaosimama usikuKatika nyumba ya BWANA.

2. Painulieni patakatifu mikono yenu,Na kumhimidi BWANA.