1. Msingi wake upoJuu ya milima mitakatifu.
2. BWANA ayapenda malango ya SayuniKuliko maskani zote za Yakobo.
3. Umetajwa kwa mambo matukufu,Ee Mji wa Mungu.
4. Nitataja Rahabu na BabeliMiongoni mwao wanaonijua.Tazama Filisti, na Tiro, na Kushi;Huyu alizaliwa humo.
5. Naam, mintarafu Sayuni itasemwa,Huyu na huyu alizaliwa humo.Na Yeye Aliye juuAtaufanya imara.
6. BWANA atahesabu, awaandikapo mataifa,Huyu alizaliwa humo.