Zab. 23 Swahili Union Version (SUV)

Mchungaji Mwema

1. BWANA ndiye mchungaji wangu,Sitapungukiwa na kitu.

2. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

3. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongozaKatika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

4. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,Sitaogopa mabaya;Kwa maana Wewe upo pamoja nami,Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

5. Waandaa meza mbele yangu,Machoni pa watesi wangu.Umenipaka mafuta kichwani pangu,Na kikombe changu kinafurika.