1. Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu;Katikati ya miungu anahukumu.
2. Hata lini mtahukumu kwa dhuluma,Na kuzikubali nyuso za wabaya?
3. Mfanyieni hukumu maskini na yatima;Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara;
4. Mwokoeni maskini na mhitaji;Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.
5. Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani;Misingi yote ya nchi imetikisika.
6. Mimi nimesema, Ndinyi miungu,Na wana wa Aliye juu, nyote pia.
7. Lakini mtakufa kama wanadamu,Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.