Zab. 3 Swahili Union Version (SUV)

Mwamini Mungu katika Dhiki

1. BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi,Ni wengi wanaonishambulia,

2. Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu,Hana wokovu huyu kwa Mungu.

3. Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote,Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.

4. Kwa sauti yangu namwita BWANANaye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.

5. Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka,Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.

6. Sitayaogopa makumi elfu ya watu,Waliojipanga juu yangu pande zote.

7. BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe,Maana umewapiga taya adui zangu wote;Umewavunja meno wasio haki.