Zab. 67 Swahili Union Version (SUV)

Mataifa Yaitwa Kumsifu Mungu

1. Mungu na atufadhili na kutubariki,Na kutuangazia uso wake.

2. Njia yake ijulike duniani,Wokovu wake katikati ya mataifa yote.

3. Watu na wakushukuru, Ee Mungu,Watu wote na wakushukuru.

4. Mataifa na washangilie,Naam, waimbe kwa furaha,Maana kwa haki utawahukumu watu,Na kuwaongoza mataifa walioko duniani.

5. Watu na wakushukuru, Ee Mungu,Watu wote na wakushukuru.

6. Nchi imetoa mazao yakeMUNGU, Mungu wetu, ametubariki.