Zab. 122 Swahili Union Version (SUV)

Wimbo wa Sifa na Sala kwa Yerusalemu

1. Nalifurahi waliponiambia,Na twende nyumbani kwa BWANA.

2. Miguu yetu imesimamaNdani ya malango yako, Ee Yerusalemu.

3. Ee Yerusalemu uliyejengwaKama mji ulioshikamana,

4. Huko ndiko walikopanda kabila,Kabila za BWANA;Ushuhuda kwa Israeli,Walishukuru jina la BWANA.

5. Maana huko viliwekwa viti vya hukumu,Viti vya enzi vya mbari ya Daudi.

6. Utakieni Yerusalemu amani;Na wafanikiwe wakupendao;

7. Amani na ikae ndani ya kuta zako,Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.

8. Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zanguNiseme sasa, Amani ikae nawe.