Zab. 123 Swahili Union Version (SUV)

Ombi la Huruma

1. Nimekuinulia macho yangu,Wewe uketiye mbinguni.

2. Kama vile macho ya watumishiKwa mkono wa bwana zaoKama macho ya mjakaziKwa mkono wa bibi yake;Hivyo macho yetu humwelekea BWANA, Mungu wetu,Hata atakapoturehemu.

3. Uturehemu, Ee BWANA, uturehemu sisi,Kwa maana tumeshiba dharau.