Zab. 30 Swahili Union Version (SUV)

Shukrani kwa Kuponywa Maradhi Mabaya

1. Ee BWANA, nitakutukuza kwa maana umeniinua,Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu.

2. Ee BWANA, Mungu wangu,Nalikulilia ukaniponya.

3. Umeniinua nafsi yangu,Ee BWANA, kutoka kuzimu.Umenihuisha na kunitoaMiongoni mwao washukao shimoni.

4. Mwimbieni BWANA zaburi,Enyi watauwa wake.Na kufanya shukrani.Kwa kumbukumbu la utakatifu wake.

5. Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo,Katika radhi yake mna uhai.Huenda kilio huja kukaa usiku,Lakini asubuhi huwa furaha.

6. Nami nilipofanikiwa nalisema,Sitaondoshwa milele.

7. BWANA, kwa radhi yakoWewe uliuimarisha mlima wangu.Uliuficha uso wako,Nami nikafadhaika.

8. Ee BWANA, nalikulilia Wewe,Naam, kwa BWANA naliomba dua.

9. Mna faida gani katika damu yanguNishukapo shimoni?Mavumbi yatakusifu?Yataitangaza kweli yako?

10. Ee BWANA, usikie, unirehemu,BWANA, uwe msaidizi wangu.

11. Uligeuza matanga yangu kuwa machezo;Ulinivua gunia, ukanivika furaha.