1. Mfanyieni BWANA shangwe, dunia yote;
2. Mtumikieni BWANA kwa furaha;Njoni mbele zake kwa kuimba;
3. Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu;Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
4. Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;Nyuani mwake kwa kusifu;Mshukuruni, lihimidini jina lake;