Zab. 93 Swahili Union Version (SUV)

Ukuu wa Enzi ya Mungu

1. BWANA ametamalaki, amejivika adhama,BWANA amejivika, na kujikaza nguvu.Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;

2. Kiti chako kimekuwa thabiti tokea zamani;Wewe ndiwe uliye tangu milele.

3. Ee BWANA, mito imepaza,Mito imepaza sauti zake,Mito imepaza uvumi wake.

4. Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu,Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo,BWANA Aliye juu ndiye mwenye ukuu.