Zab. 8 Swahili Union Version (SUV)

Utukufu wa Mungu na Hadhi ya Utu

1. Wewe, MUNGU, Bwana wetuJinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;

2. Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyaoUmeiweka misingi ya nguvu;Kwa sababu yao wanaoshindana nawe;Uwakomeshe adui na mijilipiza kisasi.

3. Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako,Mwezi na nyota ulizoziratibisha;

4. Mtu ni kitu gani hata umkumbuke,Na binadamu hata umwangalie?

5. Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu;Umemvika taji ya utukufu na heshima;

6. Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.

7. Kondoo, na ng’ombe wote pia;Naam, na wanyama wa kondeni;

8. Ndege wa angani, na samaki wa baharini;Na kila kipitacho njia za baharini.