1. Haleluya.Msifuni Mungu katika patakatifu pake;Msifuni katika anga la uweza wake.
2. Msifuni kwa matendo yake makuu;Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3. Msifuni kwa mvumo wa baragumu;Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4. Msifuni kwa matari na kucheza;Msifuni kwa zeze na filimbi;
5. Msifuni kwa matoazi yaliayo;Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6. Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA.Haleluya.