1. BWANA, ni nani atakayekaaKatika hema yako?Ni nani atakayefanya maskani yakeKatika kilima chako kitakatifu?
2. Ni mtu aendaye kwa ukamilifu,Na kutenda haki.Asemaye kweli kwa moyo wake,
3. Asiyesingizia kwa ulimi wake.Wala hakumtenda mwenziwe mabaya,Wala hakumsengenya jirani yake.
4. Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa,Bali huwaheshimu wamchao BWANAIngawa ameapa kwa hasara yake,Hayabadili maneno yake.