1. Ee Bwana, unihukumu, unitetee kwa taifa lisilo haki,Uniokoe na mtu wa hila asiye haki.
2. Kwa kuwa Wewe ndiwe Mungu uliye nguvu zangu; kwa nini umenitupa?Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?
3. Niletewe nuru yako na kweli yako ziniongoze,Zinifikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata maskani yako.
4. Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliyefuraha yangu na shangwe yangu;Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu.