1. Nitayainua macho yangu niitazame milima,Msaada wangu utatoka wapi?
2. Msaada wangu u katika BWANA,Aliyezifanya mbingu na nchi.
3. Asiuache mguu wako usogezwe;Asisinzie akulindaye;
4. Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi,Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
5. BWANA ndiye mlinzi wako;BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume.
6. Jua halitakupiga mchana,Wala mwezi wakati wa usiku.
7. BWANA atakulinda na mabaya yote,Atakulinda nafsi yako.