1. Rehema na hukumu nitaziimba,Ee BWANA, nitakuimbia zaburi.
2. Nitaiangalia njia ya unyofu;Utakuja kwangu lini?Nitakwenda kwa unyofu wa moyoNdani ya nyumba yangu.
3. Sitaweka mbele ya macho yanguNeno la uovu.Kazi yao waliopotoka naichukia,Haitaambatana nami.
4. Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu,Lililo ovu sitalijua.
5. Amsingiziaye jirani yake kwa siri,Huyo nitamharibu.Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno,Huyo sitavumilia naye.
6. Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,Hao wakae nami.Yeye aendaye katika njia kamilifu,Ndiye atakayenitumikia.
7. Hatakaa ndani ya nyumba yanguMtu atendaye hila.Asemaye uongo hatathibitikaMbele ya macho yangu.