Zab. 126 Swahili Union Version (SUV)

Mavuno ya Shangwe

1. BWANA alipowarejeza mateka wa Sayuni,Tulikuwa kama waotao ndoto.

2. Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko,Na ulimi wetu kelele za furaha.Ndipo waliposema katika mataifa,BWANA amewatendea mambo makuu.

3. BWANA alitutendea mambo makuu,Tulikuwa tukifurahi.

4. Ee BWANA, uwarejeze watu wetu waliofungwa,Kama vijito vya Kusini.

5. Wapandao kwa machoziWatavuna kwa kelele za furaha.