1. Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe,Na kwa uweza wako unifanyie hukumu.
2. Ee Mungu, uyasikie maombi yangu,Uyasikilize maneno ya kinywa changu.
3. Kwa maana wageni wamenishambulia;Watu watishao wananitafuta nafsi yangu;Hawakumweka Mungu mbele yao.
4. Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia;Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.
5. Atawarudishia adui zangu ubaya wao;Uwaangamize kwa uaminifu wako.
6. Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu;Ee BWANA, nitalishukuru jina lako, maana ni jema.