Zab. 133 Swahili Union Version (SUV)

Baraka za kuwa na Umoja

1. Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza,Ndugu wakae pamoja, kwa umoja.

2. Ni kama mafuta mazuri kichwani,Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni,Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.