Zab. 70 Swahili Union Version (SUV)

Sala ya Ukombozi kutoka kwa Adui

1. Ee Mungu, uniokoe,Ee BWANA, unisaidie hima.

2. Waaibike, wafedheheke,Wanaoitafuta nafsi yangu.Warudishwe nyuma, watahayarishwe,Wapendezwao na shari yangu.

3. Warudi nyuma, na iwe aibu yao,Wanaosema, Ewe! Ewe!

4. Washangilie, wakufurahie,Wote wakutafutao.Waupendao wokovu wakoWaseme daima, Atukuzwe Mungu.