Zab. 112 Swahili Union Version (SUV)

Baraka za Mwenye Haki

1. Haleluya.Heri mtu yule amchaye BWANA,Apendezwaye sana na maagizo yake.

2. Wazao wake watakuwa hodari duniani;Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa.

3. Nyumbani mwake mna utajiri na mali,Na haki yake yakaa milele.

4. Nuru huwazukia wenye adili gizani;Ana fadhili na huruma na haki.

5. Heri atendaye fadhili na kukopesha;Atengenezaye mambo yake kwa haki.

6. Kwa maana hataondoshwa kamwe;Mwenye haki atakumbukwa milele.

7. Hataogopa habari mbaya;Moyo wake u imara ukimtumaini BWANA.

8. Moyo wake umethibitika hataogopa,Hata awaone watesi wake wameshindwa.

9. Amekirimu, na kuwapa maskini,Haki yake yakaa milele,Pembe yake itatukuzwa kwa utukufu.