1. Ndipo Debora, na Baraka mwana wa Abinoamu, wakaimba siku ile, wakisema;
2. Kwa sababu wakuu walitangulia katika Israeli,Kwa sababu watu walijitoa nafsi zao kwa hiari yao,Mhimidini BWANA.
3. Sikieni, enyi wafalme; tegeni masikio, enyi wakuu;Mimi, naam mimi, nitamwimbia BWANA;Nitamhimidi BWANA, Mungu wa Israeli.
4. BWANA, ulipotoka katika Seiri,Ulipokwenda vitani kutoka mashamba ya Edomu,Nchi ilitetema, mbingu nazo zikadondoza maji,Naam, mawingu yakadondoza maji.
5. Milima ikayeyuka mbele za uso wa BWANA,Naam hata Sinai ule mbele za uso wa BWANA, Mungu wa Israeli.
6. Katika siku za Shamgari, mwana wa Anathi,Siku za Yaeli, njia kuu zilikuwa hazina watu;Nao wenye kusafiri walipita kwa njia za kando.
7. Maliwali walikoma katika Israeli, walikoma,Hata mimi Debora nilipoinuka,Nilipoinuka mimi, mama katika Israeli.
8. Walichagua miungu mipya,Ndipo kulikuwa na vita malangoni;Je! Ilionekana ngao au mkukiKatika watu elfu arobaini wa Israeli?
9. Moyo wangu unawaelekea maliwali wa Israeli,Waliojitoa nafsi zao kwa hiari yao miongoni mwa watu;Mhimidini BWANA.
10. Itangazeni habari, ninyi mpandao punda weupe,Ninyi mketio juu ya mazulia ya thamani,Na ninyi mnaopita njiani kwa miguu.
11. Mbali na kelele za hao wapigao mishale, katika mahali pa kuteka maji,Hapo watatangaza matendo ya haki ya BWANA;Naam, matendo ya haki ya kutawala kwake katika Israeli.Ndipo watu wa BWANA waliposhuka malangoni.
12. Amka, amka, Debora;Amka, amka, imba wimbo.Inuka, Baraka, wachukue mateka waoWaliokuchukua mateka, Ee mwana wa Abinoamu.
13. Ndipo walitelemka mabaki ya waungwana na ya watu;BWANA alishuka kwa ajili yangu apigane na mashujaa.
14. Kutoka Efraimu walitelemka wao ambao shina lao ni katika Amaleki,Nyuma yako, Benyamini, kati ya watu wako.Kutoka Makiri walishuka maliwali,Na kutoka Zabuloni wao washikao fimbo ya mwandishi.
15. Na wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora.Kama alivyokuwa Isakari, ndivyo alivyokuwa Baraka.Waliingia bondeni kwa kasi miguuni pake.Kwenye vijito vya ReubeniPalikuwa na makusudi makuu mioyoni.
16. Mbona ulikaa katika mazizi ya kondoo,Kusikiliza filimbi zipigwazo ili kuita makundi?Kwenye vijito vya ReubeniPalikuwa na makusudi makuu mioyoni.