Hes. 24:5-18 Swahili Union Version (SUV)

5. Mahema yako ni mazuri namna gani, Ee Yakobo,Maskani zako, Ee Israeli!

6. Mfano wa bonde zimetandwa,Mfano wa bustani kando ya mto,Mfano wa mishubiri aliyoipanda BWANA,Mfano wa mierezi kando ya maji.

7. Maji yatafurika katika ndoo zake,Na mbegu zake zitakuwa katika maji mengi.Na mfalme wake ataadhimishwa kuliko Agagi,Na ufalme wake utatukuzwa.

8. Mungu amemleta kutoka Misri,Ana nguvu mfano wa nguvu za nyati;Atawameza mataifa walio adui zake,Ataivunja mifupa yao vipande vipande.Atawachoma kwa mishale yake.

9. Aliinama, akalala mfano wa simba,Na kama simba mke; ni nani atakayemstusha?Na abarikiwe kila akubarikiye,Na alaaniwe kila akulaaniye.

10. Hasira ya Balaki ikawaka juu ya Balaamu akayapiga makofi; Balaki akamwambia Balaamu, Nalikuita ili unilaanie adui zangu, na tazama, umewabariki kabisa mara tatu hizi.

11. Basi sasa kimbilia mahali pako; naliazimu kukuheshimu sana; lakini, tazama, BWANA amekuzuilia heshima.

12. Balaamu akamwambia Balaki, Je! Sikuwaambia wajumbe wako ulionipelekea, nikisema,

13. Kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kupita mpaka wa neno la BWANA, kutenda neno jema, wala neno baya, kwa nia yangu mwenyewe; BWANA atakalolinena ndilo nitakalolinena mimi.

14. Basi sasa, tazama, ninakwenda kwa watu wangu; haya, nitakuarifu mambo ambayo watu hawa watakayowatenda watu wako siku za mwisho.

15. Akatunga mithali yake akasema,Balaamu mwana wa Beori asema,Yule mtu aliyefumbwa macho asema,

16. Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu,Na kuyajua maarifa yake Aliye Juu.Yeye aonaye maono ya Mwenyezi,Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho,

17. Namwona, lakini si sasa;Namtazama, lakini si karibu;Nyota itatokea katika YakoboNa fimbo ya enzi itainuka katika Israeli;Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu,Na kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia.

18. Na Edomu itakuwa milkiSeiri pia itakuwa milki, waliokuwa adui zake;Israeli watakapotenda kwa ushujaa.

Hes. 24