Wim. 4:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Tazama, u mzuri, mpenzi wangu,U mzuri, macho yako ni kama ya hua,Nyuma ya barakoa yako.Nywele zako ni kama kundi la mbuzi,Wakijilaza mbavuni pa mlima Gileadi.

2. Meno yako ni kama kundi waliokatwa manyoya,Wakipanda kutoka kuoshwa,Ambao kila mmoja amezaa mapacha,Wala hakuna aliyefiwa kati yao.

3. Midomo yako ni kama uzi mwekundu,Na kinywa chako ni kizuri;Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga,Nyuma ya barakoa yako.

4. Shingo yako ni kama mnara wa Daudi,Uliojengwa pa kuwekea silaha;Ngao elfu zimetungikwa juu yake,Zote ni ngao za mashujaa.

5. Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili,Nyuma ya barakoa yako.Ambao ni mapacha ya paa;Wakilisha penye nyinyoro.

6. Hata jua lipunge, na vivuli vikimbie,Nitakwenda kwenye mlima wa manemane,Na kwenye kilima cha ubani.

7. Mpenzi wangu, u mzuri pia pia,Wala ndani yako hamna ila.

Wim. 4