Omb. 2:10-21 Swahili Union Version (SUV)

10. Wazee wa binti Sayuni huketi chini,Hunyamaza kimya;Wametupa mavumbi juu ya vichwa vyao,Wamejivika viunoni nguo za magunia;Wanawali wa Yerusalemu huinama vichwa vyaoKuielekea nchi.

11. Macho yangu yamechoka kwa machozi,Mtima wangu umetaabika;Ini langu linamiminwa juu ya nchiKwa uharibifu wa binti ya watu wangu;Kwa sababu watoto wachanga na wanyonyao,Huzimia katika mitaa ya mji.

12. Wao huwauliza mama zao,Zi wapi nafaka na divai?Hapo wazimiapo kama waliojeruhiwaKatika mitaa ya mji,Hapo walipomiminika nafsi zaoVifuani mwa mama zao.

13. Nikushuhudie nini? Nikufananishe na nini,Ee Binti Yerusalemu?Nikusawazishe na nini, nipate kukufariji,Ee bikira binti Sayuni?Kwa maana uvunjifu wako ni mkuu kama bahari,Ni nani awezaye kukuponya?

14. Manabii wako wameona maono kwa ajili yakoYa ubatili na upumbavuWala hawakufunua uovu wako,Wapate kurudisha kufungwa kwako;Bali wameona mabashiri ya ubatili kwa ajili yakoNa sababu za kuhamishwa.

15. Hao watu wote wapitaoHukupigia makofi;Humzomea binti Yerusalemu,Na kutikisa vichwa vyao;Je! Mji huu ndio ulioitwa, Ukamilifu wa uzuri,Furaha ya dunia yote?

16. Juu yako adui zako woteWamepanua vinywa vyao;Huzomea, husaga meno yao,Husema, Tumemmeza;Hakika siku hii ndiyo tuliyoitazamia;Tumeipata, tumeiona.

17. BWANA ameyatenda aliyoyakusudia; amelitimiza neno lake,Aliloliamuru siku za kale;Ameangusha hata chini,Wala hakuona huruma;Naye amemfurahisha adui juu yako,Ameitukuza pembe ya watesi wako.

18. Mioyo yao ilimlilia Bwana;Ee ukuta wa binti Sayuni!Machozi na yachuruzike kama mtoMchana na usiku;Usijipatie kupumzika;Mboni ya jicho lako isikome.

19. Inuka, ulalamike usiku,Mwanzo wa makesha yake;Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana;Umwinulie mikono yako;Kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa,Mwanzo wa kila njia kuu.

20. Tazama, BWANA, uangalie,Ni nani uliyemtenda hayo!Je! Wanawake wale mazao yao,Watoto waliowabeba?Je! Kuhani na nabii wauaweKatika patakatifu pa Bwana?

21. Kijana na mzee hulala chiniKatika njia kuu;Wasichana wangu na wavulana wanguWameanguka kwa upanga;Umewaua katika siku ya hasira yako;Umeua, wala hukuona huruma.

Omb. 2