1. Jinsi mji huu ukaavyo ukiwa,Huo uliokuwa umejaa watu!Jinsi alivyokuwa kama mjane,Yeye aliyekuwa mkuu kati ya mataifa!Binti mfalme kati ya majimbo,Jinsi alivyoshikwa shokoa!
2. Hulia sana wakati wa usiku,Na machozi yake yapo mashavuni;Miongoni mwa wote waliompendaHakuna hata mmoja amfarijiye;Rafiki zake wote wamemtenda hila,Wamekuwa adui zake.
3. Yuda amehamishwa kwa sababu ya kuonewa,Na kwa sababu ya utumwa mkuu;Anakaa kati ya makafiri,Haoni raha iwayo yote;Wote waliomfuata wamempataKatika dhiki yake.
4. Njia za Sayuni zaomboleza,Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu;Malango yake yote yamekuwa ukiwa,Makuhani wake hupiga kite;Wanawali wake wanahuzunika;Na yeye mwenyewe huona uchungu.
5. Watesi wake wamekuwa kichwa,Adui zake hufanikiwa;Kwa kuwa BWANA amemtesaKwa sababu ya wingi wa makosa yake;Watoto wake wadogo wamechukuliwa matekaMbele yake huyo mtesi.
6. Naye huyo binti SayuniEnzi yake yote imemwacha;Wakuu wake wamekuwa kama ayalaWasioona malisho;Nao wamekwenda zao hawana nguvuMbele yake anayewafuatia.
7. Siku za mateso na misiba yake,Yerusalemu huyakumbuka matamaniko yake yoteYaliyokuwa tangu siku za kale;Hapo watu wake walipoanguka mikononi mwa mtesi,Wala hakuna hata mmoja wa kumsaidia;Hao watesi wake walimwona,Wakafanya sabato zake kuwa mzaha.
8. Yerusalemu amefanya dhambi sana;Kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu;Wote waliomheshimu wanamdharau,Kwa sababu wameuona uchi wake;Naam, yeye anaugua,Na kujigeuza aende nyuma.