Yerusalemu amefanya dhambi sana;Kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu;Wote waliomheshimu wanamdharau,Kwa sababu wameuona uchi wake;Naam, yeye anaugua,Na kujigeuza aende nyuma.