Hulia sana wakati wa usiku,Na machozi yake yapo mashavuni;Miongoni mwa wote waliompendaHakuna hata mmoja amfarijiye;Rafiki zake wote wamemtenda hila,Wamekuwa adui zake.