5. Akawa mfalme katika Yeshuruni,Walipokutanika wakuu wa watu,Makabila yote ya Israeli pamoja.
6. Reubeni na aishi, asife;Lakini watu wake na wawe wachache.
7. Na baraka ya Yuda ni hii; akasema,Isikize, Ee BWANA, sauti ya Yuda,Umlete ndani kwa watu wake;Alijitetea kwa mikono yake;Nawe utakuwa msaada juu ya adui zake.
8. Akamnena Lawi,Thumimu yako na Urimu yako vina mtakatifu wako,Uliyemjaribu huko Masa;Ukateta naye kwenye maji ya Meriba.
9. Aliyemtaja baba yake na mama yake, Mimi sikumwona;Wala nduguze hakuwakubali;Wala hakuwajua watoto wake mwenyewe;Maana wameliangalia neno lako,Wamelishika agano lako.
10. Watamfundisha Yakobo hukumu zako,Na Israeli torati yako,Wataweka uvumba mbele zako,Na sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni mwako.
11. Ee BWANA, ubariki mali zake,Utakabali kazi ya mikono yake;Uwapige viuno vyao waondokao juu yake,Na wenye kumchukia, wasiinuke tena.
12. Akamnena Benyamini,Mpenzi wa BWANA atakaa salama kwake;Yuamfunika mchana kutwa,Naye hukaa kati ya mabega yake.
13. Na Yusufu akamnena,Nchi yake na ibarikiwe na BWANA;Kwa vitu vya thamani vya mbinguni, kwa huo umande,Na kwa kilindi kilalacho chini,