Isa. 60:16-22 Swahili Union Version (SUV)

16. Utanyonya maziwa ya mataifa,Utanyonya matiti ya wafalme;Nawe utajua ya kuwa mimi, BWANA, ni mwokozi wako,Na mkombozi wako, Mwenye enzi wa Yakobo.

17. Badala ya shaba nitaleta dhahabu,Na badala; ya chuma nitaleta fedha,Na badala ya mti, shaba,Na badala ya mawe, chuma;Tena nitawafanya wasimamizi wako wawe amani,Na hao wakutozao fedha kuwa haki.

18. Jeuri haitasikiwa tena katika nchi yako,Ukiwa na uharibifu hazitakuwa mipakani mwako;Bali utaziita kuta zako, Wokovu,Na malango yako, Sifa.

19. Jua halitakuwa nuru yako tena wakati wa mchana,Wala mwezi hautakupa nuru kwa mwangaza wake;Bali BWANA atakuwa nuru ya milele kwako,Na Mungu wako atakuwa utukufu wako.

20. Jua lako halitashuka tena,Wala mwezi wako hautajitenga;Kwa kuwa BWANA mwenyewe atakuwa nuru yako ya milele;Na siku za kuomboleza kwako zitakoma.

21. Watu wako nao watakuwa wenye haki wote,Nao watairithi nchi milele;Chipukizi nililolipanda mimi mwenyewe,Kazi ya mikono yangu mwenyewe,Ili mimi nitukuzwe.

22. Mdogo atakuwa elfu,Na mnyonge atakuwa taifa hodari;Mimi, BWANA, nitayahimiza hayo wakati wake.

Isa. 60