15. Niseme nini? Yeye amenena nami,na yeye mwenyewe ametenda hayo;Nitakwenda polepole miaka yangu yote,kwa sababu ya uchungu wa nafsi yangu.
16. Ee Bwana, kwa mambo hayo watu huishi;Na uhai wa roho yangu u katika hayo yote;Kwa hiyo uniponye na kunihuisha.
17. Tazama; nalikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu;Lakini kwa kunipenda umeniokoa na shimo la uharibifu;Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.
18. Kwa kuwa kuzimu hakuwezi kukusifu;mauti haiwezi kukuadhimisha;Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako.
19. Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo;Baba atawajulisha watoto kweli yako.
20. BWANA yu tayari kunipa wokovu.Basi, kwa vinubi tutaziimba nyimbo zangu,Siku zote za maisha yetu nyumbani mwa BWANA.
21. Maana Isaya amesema, Na watwae mkate wa tini, wakauweke juu ya jipu, naye atapona.
22. Tena Hezekia alikuwa amesema, Iko ishara gani ya kunionyesha ya kuwa nitapanda niingie nyumbani mwa BWANA?