Isa. 25:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Ee BWANA, wewe u Mungu wangu;Nitakutukuza na kulihimidi jina lako;Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu,Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.

2. Kwa sababu umefanya mji kuwa ni chungu;Mji wenye boma kuwa ni magofu;Jumba la wageni kuwa si mji;Hautajengwa tena milele.

3. Kwa hiyo watu walio hodari watakutukuza,Mji wa mataifa watishao utakuogopa.

4. Maana umekuwa ngome ya maskini,Ngome ya mhitaji katika dhiki yake,Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani,Kivuli wakati wa hari;Wakati uvumapo upepo wa watu watishao,Kama dhoruba ipigayo ukuta.

5. Kama vile hari katika mahali pakavuUtaushusha mshindo wa wageni;Kama ilivyo hari kwa kivuli cha wingu,Wimbo wa hao watishao utashushwa.

Isa. 25