33. Ndipo mfalme akamwomboleza Abneri, akasema,Ilimpasaje Abneri kufa afavyo mpumbavu?
34. Mikono yako haikufungwa,Wala miguu yako haikutiwa pingu;Aangukavyo mtu mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka.Na watu wote wakaongeza kumlilia.
35. Wakaja na watu wote wamshurutishe Daudi kula chakula, ukalipo bado mchana; lakini Daudi akaapa, akasema Mungu anitendee vivyo, na kuzidi, nikionja mkate, au kingine cho chote kabla lichwapo jua.
36. Wakaangalia watu wote, yakawa mema machoni pao; kama yalivyokuwa mema machoni pao yote aliyoyatenda mfalme.
37. Wakajua watu wote, na Israeli wote, siku ile, ya kuwa si nia ya mfalme kwamba auawe Abneri, mwana wa Neri.
38. Kisha mfalme akawaambia watumishi wake, Hamjui ya kuwa mkuu mmoja, naye ni mtu mkubwa ameanguka leo katika Israeli?
39. Nami leo nimedhoofika, hata nijapotiwa mafuta niwe mfalme; na watu hao, wana wa Seruya, ni wagumu kwangu mimi; BWANA amlipie mwovu sawasawa na uovu wake.