Zab. 71:17-23 Swahili Union Version (SUV)

17. Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu;Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo.

18. Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi,Ee Mungu, usiniache.Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako,Na kila atakayekuja uweza wako.

19. Na haki yako, Ee Mungu,Imefika juu sana.Wewe uliyefanya mambo makuu;Ee Mungu, ni nani aliye kama Wewe?

20. Wewe, uliyetuonyesha mateso mengi, mabaya,Utatuhuisha tena.Utatupandisha juu tenaTokea pande za chini ya nchi.

21. Laiti ungeniongezea ukuu!Urejee tena na kunifariji moyo.

22. Nami nitakushukuru kwa kinanda,Na kweli yako, Ee Mungu wangu.Nitakuimbia Wewe kwa kinubi,Ee Mtakatifu wa Israeli.

23. Midomo yangu itafurahi sana nikuimbiapo,Na nafsi yangu uliyoikomboa.

Zab. 71