1. Tazama, u mzuri, mpenzi wangu,U mzuri, macho yako ni kama ya hua,Nyuma ya barakoa yako.Nywele zako ni kama kundi la mbuzi,Wakijilaza mbavuni pa mlima Gileadi.
2. Meno yako ni kama kundi waliokatwa manyoya,Wakipanda kutoka kuoshwa,Ambao kila mmoja amezaa mapacha,Wala hakuna aliyefiwa kati yao.
3. Midomo yako ni kama uzi mwekundu,Na kinywa chako ni kizuri;Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga,Nyuma ya barakoa yako.
4. Shingo yako ni kama mnara wa Daudi,Uliojengwa pa kuwekea silaha;Ngao elfu zimetungikwa juu yake,Zote ni ngao za mashujaa.