4. Njia za Sayuni zaomboleza,Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu;Malango yake yote yamekuwa ukiwa,Makuhani wake hupiga kite;Wanawali wake wanahuzunika;Na yeye mwenyewe huona uchungu.
5. Watesi wake wamekuwa kichwa,Adui zake hufanikiwa;Kwa kuwa BWANA amemtesaKwa sababu ya wingi wa makosa yake;Watoto wake wadogo wamechukuliwa matekaMbele yake huyo mtesi.
6. Naye huyo binti SayuniEnzi yake yote imemwacha;Wakuu wake wamekuwa kama ayalaWasioona malisho;Nao wamekwenda zao hawana nguvuMbele yake anayewafuatia.
7. Siku za mateso na misiba yake,Yerusalemu huyakumbuka matamaniko yake yoteYaliyokuwa tangu siku za kale;Hapo watu wake walipoanguka mikononi mwa mtesi,Wala hakuna hata mmoja wa kumsaidia;Hao watesi wake walimwona,Wakafanya sabato zake kuwa mzaha.
8. Yerusalemu amefanya dhambi sana;Kwa hiyo amekuwa kama kitu kichafu;Wote waliomheshimu wanamdharau,Kwa sababu wameuona uchi wake;Naam, yeye anaugua,Na kujigeuza aende nyuma.
9. Uchafu wake ulikuwa katika marinda yake;Hakukumbuka mwisho wake;Kwa hiyo ameshuka kwa ajabu;Yeye hana mtu wa kumfariji;Tazama, BWANA, teso langu;Maana huyo adui amejitukuza.
10. Huyo mtesi amenyosha mkono wakeJuu ya matamaniko yake yote;Maana ameona ya kuwa makafiri wameingiaNdani ya patakatifu pake;Ambao kwa habari zao wewe uliamuruWasiingie katika kusanyiko lako.