Isa. 5:26-30 Swahili Union Version (SUV)

26. Naye atawatwekea bendera mataifa toka mbali,Naye atawapigia miunzi tokea mwisho wa nchi;Na tazama, watakuja mbio mbio upesi sana.

27. Miongoni mwao hakuna achokaye wala kukwaa;Hakuna asinziaye wala kulala usingizi;Wala mshipi wa viuno vyao hautalegea.Wala ukanda wa viatu vyao hautakatika;

28. Mishale yao ni mikali, na pindi zao zote zimepindika;Kwato za farasi zao zitahesabika kama gumegume;Na gurudumu zao kama kisulisuli;

29. Ngurumo yao itakuwa kama ya simba;Watanguruma kama wana-simba;Naam, watanguruma na kukamata mateka,Na kuyachukua na kwenda zao salama,Wala hakuna mtu atakayeokoa.

30. Nao watanguruma juu yao siku hiyoKama ngurumo ya bahari;Na mtu akiitazama nchi, ataona giza na dhikiNayo nuru imetiwa giza katika mawingu yake.

Isa. 5