13. Ndipo walitelemka mabaki ya waungwana na ya watu;BWANA alishuka kwa ajili yangu apigane na mashujaa.
14. Kutoka Efraimu walitelemka wao ambao shina lao ni katika Amaleki,Nyuma yako, Benyamini, kati ya watu wako.Kutoka Makiri walishuka maliwali,Na kutoka Zabuloni wao washikao fimbo ya mwandishi.
15. Na wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora.Kama alivyokuwa Isakari, ndivyo alivyokuwa Baraka.Waliingia bondeni kwa kasi miguuni pake.Kwenye vijito vya ReubeniPalikuwa na makusudi makuu mioyoni.
16. Mbona ulikaa katika mazizi ya kondoo,Kusikiliza filimbi zipigwazo ili kuita makundi?Kwenye vijito vya ReubeniPalikuwa na makusudi makuu mioyoni.
17. Gileadi alikaa ng’ambo ya Yordani,Na Dani, mbona alikaa katika merikebu?Asheri alikaa kimya penye bandari ya bahari,Alikaa katika hori zake.
18. Zabuloni ndio watu waliohatirisha roho zao hata kufa;Nao Naftali mahali palipoinuka kondeni.
19. Wafalme walikuja wakafanya vita,Ndipo wafalme wa Kanaani walifanya vita.Katika Taanaki, karibu na maji ya Megido;Hawakupata faida yo yote ya fedha.
20. Walipigana kutoka mbinguni,Nyota katika miendo yao zilipigana na Sisera.
21. Mto ule wa Kishoni uliwachukua,Ule mto wa zamani, mto wa Kishoni.Ee roho yangu, endelea mbele kwa nguvu.