2 Sam. 3:28-34 Swahili Union Version (SUV)

28. Hata baadaye Daudi aliposikia, akasema, Mimi na ufalme wangu hatuna hatia milele mbele za BWANA, kwa sababu ya damu ya Abneri, mwana wa Neri;

29. na imwangukie Yoabu kichwani pake, na nyumba yote ya babaye, tena hiyo nyumba ya Yoabu isikose kuwa na mtu mwenye kutoka damu, au aliye na ukoma, au mwenye kutegemea fimbo, au mwenye kuanguka kwa upanga au mwenye kuhitaji chakula.

30. Basi Yoabu, na Abishai nduguye, walimwua Abneri, kwa sababu yeye alimwua ndugu yao Asaheli katika vita huko Gibeoni.

31. Kisha Daudi alimwambia Yoabu, na watu wote waliokuwa pamoja naye, Rarueni nguo zenu, mkajivike nguo za magunia, mkamlilie Abneri. Naye mfalme Daudi akaifuata jeneza.

32. Wakamzika Abneri katika Hebroni; naye mfalme akapaza sauti yake, akalia kaburini kwa Abneri, nao watu wote wakalia.

33. Ndipo mfalme akamwomboleza Abneri, akasema,Ilimpasaje Abneri kufa afavyo mpumbavu?

34. Mikono yako haikufungwa,Wala miguu yako haikutiwa pingu;Aangukavyo mtu mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka.Na watu wote wakaongeza kumlilia.

2 Sam. 3