2. Mwenyezi-Mungu aliambia taifa la Edomu:“Nitakufanya mdogo miongoni mwa mataifa,utadharauliwa kabisa na wote.
3. Kiburi chako kimekudanganya:Kwa kuwa mji wako mkuu ni ngome ya miamba imarana makao yako yapo juu milimani,hivyo wajisemea,‘Nani awezaye kunishusha chini?’
4. Hata ukiruka juu kama tai,ukafanya makao yako kati ya nyota,mimi nitakushusha chini tu.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.
5. “Kama wezi au wanyang'anyi wangekujia usiku,je, wasingechukua tu kiasi cha kuwatosha?Ikiwa wavunaji zabibu wangekujia,je, wasingekuachia kiasi kidogo tu?Lakini wewe, adui zako wamekuangamiza kabisa.
6. Enyi wazawa wa Esau, mali zenu zimetekwa;hazina zenu zote zimeporwa!
7. Washirika wenzenu wamewadanganya,wamewafukuza nchini mwenu.Mliopatana nao wamewashinda vitani,rafiki wa kutegemewa ndio waliokutegea mitego,nawe hukuelewa yaliyokuwa yanatendeka.
8. Mimi Mwenyezi-Mungu nakuuliza hivi:Je, siku hiyo, sitawaangamiza wenye hekima kutoka Edomuna wenye maarifa kutoka mlima Esau?