10. Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiri mataifa yote habari za amani; na mamlaka yake yatakuwa toka bahari hata bahari, na toka Mto hata miisho ya dunia.
11. Na kwa habari zako wewe, kwa sababu ya damu ya agano lako, nimewatoa wafungwa wako katika shimo lile lisilo na maji.
12. Irudieni ngome, enyi wafungwa wa tumaini; hata hivi leo nasema ya kwamba nitakurudishia maradufu.
13. Maana nimejipindia Yuda, nimeujaza upinde wangu Efraimu; nami nitawaondokesha wana wako, Ee Sayuni, wapigane na wana wako, Ee Uyunani, nami nitakufanya wewe kuwa kama upanga wa shujaa.
14. Naye BWANA ataonekana juu yao,Na mshale wake utatoka kama umeme;Na Bwana MUNGU ataipiga tarumbeta,Naye atakwenda kwa pepo za kisulisuli za kusini.
15. BWANA wa majeshi atawalinda;Nao watakula na kuyakanyaga mawe ya teo;Nao watakunywa na kufanya kelele kama kwa divai;Nao watajazwa kama mabakuli, kama pembe za madhabahu.
16. Na BWANA, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo,Kama kundi la watu wake;Kwa maana watakuwa kama vito vya taji,Vikimeta-meta juu ya nchi yake.
17. Maana wema wake, jinsi ulivyo mwingi!Na uzuri wake, jinsi ulivyo mwingi!Nafaka itawasitawisha vijana wanaume,Na divai mpya vijana wanawake.