Zab. 59:12-16 Swahili Union Version (SUV)

12. Kwa dhambi ya kinywa chao,Na kwa neno la midomo yao,Wanaswe kwa kiburi chao,Kwa ajili ya kulaani na uongo wasemao.

13. Uwakomeshe kwa hasira,Uwakomeshe watoweke,Wajue ya kuwa Mungu atawala katika Yakobo,Na hata miisho ya dunia.

14. Wakati wa jioni hurudi, hulia kama mbwa,Na kuzunguka-zunguka mjini.

15. Watatanga-tanga hao wakitafuta chakula;Wasiposhiba watakesha usiku kucha.

16. Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi,Nitaziimba fadhili zako kwa furaha.Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu,Na makimbilio siku ya shida yangu.

Zab. 59